Kwa Mukhtasari
Hatimaye Miss Tanzania 2006, staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe habari hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa Sh13 milioni.
UFALME umeanguka!
Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe habari hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa Sh13 milioni.
Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti moja la Kitanzania Ijumaa Wikienda, Wema alikumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa kifahari wa Makumbusho jijini Dar es Salaam kwa kushindwa kuilipia kodi na bili kubwa ya umeme.
Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti moja la Kitanzania Ijumaa Wikienda, Wema alikumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo mtaa wa kifahari wa Makumbusho jijini Dar es Salaam kwa kushindwa kuilipia kodi na bili kubwa ya umeme.
“Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme peke yake nasikia anadaiwa zaidi ya Sh milioni nane (Sh362,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa. ”
“Sasa landilodi ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini akamtaka Wema ahame haraka kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.
Hata hivyo Wema ambaye ni mjamizito hakukosa pa kwenda baada ya kuchukuliwa nyumba nyingine na mbunge mmoja ambaye amekuwa akitoka naye kimapenzi, vyanzo mbalimbali vimezidi kueleza.
WEMA SEPETU ATIMULIWA TOKA NYUMBA ALIYODAI KANUNUA
Reviewed by Unknown
on
00:23
Rating:
Hakuna maoni: